Ngano Kama Nguzo ya Kubuni riwaya ya Walenisi

  • Omutimba C Washiali

Abstract

Kwa muda mrefu, usimulizi umehusishwa na ngano ambayo ni mojawapo ya tanzu za fasihi simulizi. Ngano hutolewa kwa nathari. Ngano ina jumla ya vipera kama vile; visasili, mighani, hekaya, visakale, ngano,  hurafa, ngano za mtanziko na visa vingine. Katika historia ya fasihi ya kiafrika, fasihi ilisimuliwa na kupitishwa kwa vizazi kwa njia ya mdomo. Hata hivyo, ilihifadhiwa katika kumbukumbu. Kuanzishwa kwa maandishi ndiko chanzo cha utanzu mpya wa fasihi andishi. Riwaya ya Kiswahili kwa hivyo, ni ngeni kwa vile ililetwa na majilio ya hati za kirumi zilizoletwa na wageni ili kutumika kuihifadhi fasihi. Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa, nathari ya kiswahili inaelekea kuwiana na hadithi za fasihi simulizi. Hata hivyo, zingine zinapinga kuwa, haupo uhusiano kati ya riwaya na ngano. Katika nyakati mbalimbali hata hivyo, kumeibuka nathari mbalimbali ambazo zimetatiza ufasiri na uhakiki wake. Kwa sababu ya nathari ya Kiswahili kuwa na umbo la ngano, yawezekana kuwa misingi ya usimulizi ipatikanayo katika ngano kutumika katika utunzi na uhakiki wa nathari ya Kiswahili. Inavyotambulika ni kwamba, ngano zina muundo maalumu ambao zinatumia kupitisha ujumbe wake na hivyo, kuna mawazo kuwa, ndani yake kuna sifa maalumu zinazoweza kutumiwa kufasiri vipengele muhimu katika nathari. Ngano ndizo aghalabu huhusishwa na miundo na maumbo ya usimulizi. Katika uhakiki wa hadithi uliokita mizizi Ulaya, wahakiki walihakiki masimulizi kifomyula. Hata hivyo, uhakiki wa nathari umejikita kwa muda mrefu kwa maudhui, wahusika na mtindo lakini umbo na muundo wake umepuuzwa. Hali hii inaathiri ufasiri na uhakiki wake. Kuna sababu ya kutalii nafasi ya sifa za ngano katika nathari ili kuzihusisha na utunzi na uhakiki wake.

References

Chacha L. M. 2004. Mwongozo wa Walenisi. Africawide Network. Nairobi.
Dundes A. 1999. Interntional Folkloristics. Rowman & Litlefield Publishers. Oxford England.
Dundes, A. 1965. The Study of Folk Lore. Englewood cliffs, NJ: Prentice Hall.
Gikandi, S. 1987. Reading the African Novel. Nairobi. Heinmann.
Kimani N. na Rocha C. 2008. Ufundishaji wa Fasihi; Nadharia na Mbinu. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation.
Lord, A. B. 1965. The Singer of Tales. New York Athenaeum.
Madumulla J. S. 1987. Juzuu 54/1 na 54/2. Jarida la TUKI. “Maendeleo ya Wahusika Katika Riwaya za Kiswahili Tanzania”. Dar es Salaam; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkangi K.1995. Walenisi. East African Educational Publishers Ltd. Nairobi.
Parcedes, A. na Baumann, R. 1974. Towards New Perspectives in Folklore. University of Texas Press.
Propp, V. 1968. The Morphology of The Folk Tale. The American Folk Society and Indiana University.
Vonyoli A. J. 2004. “Hadithi Kama Chombo cha Maudhui Katika Fasihi: Uchanganuzi wa Riwaya za Mkangi, Mafuta (1984) na Walenisi (1995).” Tasnifu ya M.A. haijachapishwa.
Published
2016-08-20