Miundo na Maumbo ya Simulizi Katika Adili na Nduguze

  • Omutimba C Washiali

Abstract

Sehemu hii, inalenga kuangazia sura za kimuundo za simulizi zinazopatikana katika riwaya ya Adili na Nduguze. Pia, inahusu uchunguzi wa nafasi ya sifa bainifu za miundo na maumbo tengamano zilizo dhahiri katika simulizi na ambazo zinapatikana katika riwaya ya Adili na Nduguze. Inalenga pia kubaini iwapo nguzo hizi za usimulizi zinaweza kuwa utaratibu wa utunzi wa riwaya. Katika kubaini ukweli huu katika riwaya ya Adili na Nduguze, nadharia ya Miundo na Maumbo tengemano ndiyo inayozingatiwa. Iliasisiwa na Parry (1902) na Lord aliyekuwa mwanafunzi wake. Iliendelezwa na kuboreshwa na Axel Olrik (1908) na Vladimir Propp (1928). Nadharia ya miundo na maumbo tengemano ni kitengo cha naratolojia lakini ikija kwa upande wa fasihi simulizi, miundo na maumbo tengemano imezingatiwa zaidi kuliko naratolojia kwa ujumla. Alan Dundes ni miongoni mwa waitifaki wa nadharia hii hivi leo. Nadharia hii inaweza kutumiwa kuhakiki ushairi au nyimbo na nathari. Kwa ajili ya kazi hii, vitengo vya nadharia hii vinavyoshugulikia kazi ya nathari ndivyo vilivyozingatiwa. Kwa hivyo, imetumika kulingana na alivyoitumia Olrik A (1908) katika uhakiki wa masimulizi ya jadi.

References

MAREJELEO
Buchler, Lia R, Selby, H. A. 1968. A Formal Study of Myth. Center for Intercultural Studies in Folk lore and Oral History Texas
Dundes A. 1999. Interntional Folkloristics. Rowman & Litlefield Publishers. Oxford England.
Dundes, A. 1965. The Study of Folk Lore. Englewood cliffs, NJ: Prentice Hall.
Kimani N. na Rocha C. 2008. Ufundishaji wa Fasihi; Nadharia na Mbinu. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation.
Lord, A. B. 1965. The Singer of Tales. New York Athenaeum.
Nelson. 1976. Diwani ya Shaaban 4 Masomo Yenye Adili. Thomas Nelson and Sons Ltd.
Ochenja R. 2008. “Maigizo kama Mbinu ya Maudhui katika riwaya mbili za Ken Walibora. Tasnifu ya M.A. haijchapishwa.
Propp, V. 1968. The Morphology of The Folk Tale. The American Folk Society and Indiana University.
Shaaban R. 1952. Adili na Nduguze. London. Macmillan Press Limited.
Todorov. 1981. Introduction to Poetics. Harvester Wheatsheaf. London.
Wafula R.M. 1989. “The Use of Allegory in Shaaban Robert’s Prose Works.” Tasnifu ya M.A. haijachapishwa.
Published
2016-06-09